Tuesday, March 18, 2014

MAISHA YA MAMA WAJANE BAADA YA WAUME ZAO KUFARIKI

Kuna wakati huwa nakaa chini na kuwaza kuhusu mambo wanayofanyiwa wajane walio wengi, Unakuta mume kwa bahati mbaya anafariki dunia  kisha mjane aliye baki anazurumiwa zile mali alizo chuma na mumewe kisha baada ya hapo kama aliachiwa nyumba, magari, mashamba vyote anakuwa hana haki navyo anarudi kuwa mtu wa kutangatanga nakuomba misaada kiukweli ni jambo linaloudhi na kuumiza jinsi akina mama wajane wanavyo nyanyasw.

  Ni kwanini mama mjane asifungue kesi?
watumishi wa umma walio wengi huwa hawafuati maadili na miiko ya kazi zao wakiwemo mahakimu, mawakili, n.k jarada litafunguliwa maakamani kesi itasikilizwa kwa pande zote lakini ikifikia maamuzi (hukumu) hakimu anaegamia upande mmojawa kumkandamiza mama mjane hata kama hakuna sababu (ushahidi) wa kutosha na ukichunguza kiundani utabaini kuwa Rushwa imetumika.....
Kwaajili ya rushwa mama mjane ananyimwa haki yake
kiukweli hii ni dhambi kubwa hata kwa MUNGU

No comments:

Post a Comment